Chatrapathi ni remake ya movie ya Kihindi ya classic ya Telugu ya 2005. Inamfuata kijana anayeitwa Shivaji ambaye maisha yake yanaharibiwa baada ya yeye na familia yake kulazimishwa kutoka kwenye jamii yao na kuingia kwenye maisha ya utumwa (bonded labour) katika mji wa Visakhapatnam.
Akiwa huko, Shivaji anajikuta akiwa katika mazingira ya uonevu mkubwa ambapo watu wake wananyanyaswa na wahalifu na viongozi wenye nguvu. Kadri anavyoishi kwenye hali hiyo, anaamua kusimama na kupigania watu wake ili kuwaokoa kutoka kwenye ukandamizaji huo.
Story inaendelea kumuonyesha Shivaji akibadilika kutoka kijana wa kawaida kuwa kiongozi mwenye nguvu anayeheshimiwa na kuogopwa na maadui zake. Hata hivyo, safari yake inakuwa ngumu zaidi pale anapopata maadui wa ndani na nje, akiwemo ndugu yake wa kambo ambaye ana chuki naye na anataka kumuangamiza.
Comments (0)
Unataka kutoa maoni yako kuhusu filamu hii?
Ingia (Sign In) Kuweka MaoniHakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!