Abigail ni movie ya horror na thriller inayofuatilia kundi la wahalifu wanaompata kazi ya kumteka mtoto mdogo wa tajiri ili kudai fidia kubwa.
Wanapompeleka kwenye jumba la kifahari lililotengwa, mambo yanaanza kubadilika ghafla pale wanapogundua kuwa huyo mtoto si wa kawaida kama walivyodhani. Badala ya wao kuwa wawindaji, wanajikuta wao ndio wanaowindwa ndani ya jumba hilo.
Kadri usiku unavyoendelea, siri za kutisha zinaanza kufichuka, na kundi hilo linapaswa kupambana kuokoa maisha yao dhidi ya nguvu isiyo ya kawaida. Ni hadithi ya hofu, mabadiliko ya ghafla, na mapambano ya kuishi.
Comments (0)
Unataka kutoa maoni yako kuhusu filamu hii?
Ingia (Sign In) Kuweka MaoniHakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!